MRADI WA KISASA HILLTOP
Watumishi Housing imeanzisha mradi mpya wa ujenzi wa nyumba; katika eneo la Kisasa Hiltop Dodoma ambapo jumla ya nyumba 500 zitajengwa katika awamu tofauti. Uamuzi huu umekuja baada ya kukamilika kwa mradi wa awali eneo la Kisasa Relini Njedengwa unaojumuisha nyumba 39 za kawaida pamoja na jengo 1 la biashara ambapo mauzo yamefanyika kwa mafanikio makubwa.
Awamu ya kwanza ya Mradi wa Kisasa Hiltop Dodoma inajumuisha nyumba 92 za chini ambapo ujenzi wake ulianza rasmi mwaka 2020 na tayari umekamilika. Hadi sasa 85% ya nyumba zote tayari zimeuzwa.
Pia kuna ongezeko la nyumba mpya 38 ambapo ujenzi wake unategemewa kukamilika mwezi Septemba 2022 na hivyo kufikisha jumla ya nyumba 130 katika mradi huu.
Na. |
Aina ya nyumba |
Idadi ya vyumba |
Meta za mraba |
Bei (bila VAT) |
Bei (ikiwa na VAT) |
1 |
Aina A |
3 |
115 |
77,118,644.00 |
98,500,000.00 |
2 |
Aina B |
3 |
85 |
63,359,322.00 |
84,500,000.00 |
3 |
Aina C |
3 |
78 |
57,627,118.00 |
79,800,000.00 |
4 |
Aina D |
3 |
68 |
45,762,712.00 |
69,800,000.00 |
5 |
Aina E |
2 |
60 |
38,824,630.51 |
45,800,000.00 |