KUHUSU WHI

WHI ni mwendelezaji wa milki na msimamizi wa mifuko ya uwekezaji aliyepewa jukumu la uanzishaji na usimamizi wa mifuko ya uwekezaji wa pamoja .

KUHUSU WHI

Watumishi Housing Investments (WHI) ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2014 chini ya sheria ya Makampuni (Cap 212) kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma na wanachama wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni matarajio katika malengo ya kitaifa na kimataifa kama yalivyoainishwa katika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi (2000), Dira ya Maendeleo ya 2025, na Malengo ya Maendeleo Endelevu:2030.
WHI inasimamia Mifuko ya Uwekezaji ambayo ni: Mfuko wa Uwekezaji katika Milki (REIT) na Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja (CIS) ambapo kwa sasa WHI inaendesha MFUKO WA FAIDA. Kwa maana hiyo, shughuli za REIT na MFUKO WA FAIDA ni kwa mujibu wa Sheria ya Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Soko la Mitaji na Dhamana (CIS) na Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha, 2006. Zaidi ya hayo, REIT pia inazingatia (Sheria za Mifuko ya Uwekezaji wa Milki), 2011.
Kutokana na majukumu yake kuwa ni pamoja na Usimamizi wa Mfuko ya Uwekezaji na Usimamizi wa Milki, WHI pia inaongozwa na sera na sheria nyingine, ambazo ni pamoja na Sera ya Taifa ya Hifadhi ya Jamii ya mwaka 2003, Sera ya Nyumba ya mwaka 2005, Sera ya Ardhi 1995 pamoja na sera nyingine mtambuka.

MAJUKUMU YA WHI

Shirika la Watumishi Housing (WHI) kama Msimamizi wa Mifuko ya Uwekezaji na Mwendelezaji wa Milki, Majukumu yake makuu ni kama ifuatavyo:

Dira Yetu

Kuwezesha Upatikanaji wa Nyumba Bora na Uhuru wa Kifedha

Dhima Yetu

Kuwawezesha wafanyakazi Kukuza Kipato na Kumiliki Nyumba Bora kupitia usimamizi wa Milki na Uwekezaji wa Pamoja

WAWEKEZAJI WA AWALI WA WHI