UJENZI PAMOJA NA HUDUMA ZA USHAURI


WHI imesajiliwa kama Mkandarasi Daraja la 1 na mshauri elekezi wa ujenzi na kupitia Idara ya Uendeshaji imefanikiwa kujenga Ofisi za Serikali na kutoa Ushauri Elekezi kama ifuatavyo:

1. Ofisi ya Rais (UTUMISHI)

WHI inatoa huduma ya ushauri elekezi katika ujenzi wa Jengo la Ofisi ya UTUMISHI eneo la Mtumba Dodoma.

2. Ujenzi wa ukuta kwa nyumba za Chuo Kikuu cha Dodoma

WHI imejenga ukuta kwa nyumba za Chuo Kikuu cha Dodoma.

3. Ujenzi wa Lango Kuu la Chuo Kikuu cha Dodoma

WHI inatoa huduma za ujenzi wa Lango Kuu la Chuo Kikuu cha Dodoma.

4. Ujenzi wa Nyumba za Watumishi – Mkulazi Dakawa

WHI inajenga nyumba za Wafanyakazi wa Kiwanda cha Sukari – Mkulanzi Dakawa

5. Ujenzi wa Maabara ya Ukaguzi na Uchunguzi

WHI imekamilisha ujenzi wa Maabara ya Ukaguzi na Uchunguzi Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Dodoma.

6. Ukarabati Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Mbeya

WHI imefanya ukarabati wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Mbeya.

7. Ukarabati Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Shinyanga

WHI inafanya Ukarabati Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi Shinyanga.

8. Ukarabati Ofisi ya Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA)

WHI imekamilisha ukarabati wa Ofisi za Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA) Jijini Mwanza.

9. Jengo la Mfuko wa Mawasiliano (UCSAF) – Dodoma

WHI imetoa ushauri elekezi katika usimamizi wa Jengo la Makao Makuu ya Mfuko wa Mawasiliano (UCSAF) Jijini Dodoma.

10. CHUO CHA UTUMISHI SINGIDA

WHI imekamilisha Ujenzi wa Jengo la Chuo cha Utumishi Singida.