WATUMISHI HOUSE MAGOMENI

Mradi wa nyumba za Ghorofa wa Jengo la Watumishi House Magomeni ulikamilika mwaka 2018 ambapo 100% ya nyumba zote zimeuzwa kwa watumishi wa umma. Mradi huu ulijumuisha nyumba za ghorofa zenye vyumba kati ya 2 na 3 vya kulala. Bei ya mwanzo ilikuwa Tsh. 88,500,000.00 (ikiwa na VAT). Kwa sasa ghorofa ya kwanza na ya chini ya Jengo zinapangishwa kwa shughuli za biashara ambapo meta 1 ya mraba inapangishwa kwa Tsh. 6,560.00 (ikwa na VAT na tozo la huduma)