MRADI WA KISASA HILLTOP

Watumishi Housing imeanzisha mradi mpya wa ujenzi wa nyumba; katika eneo la Kisasa Hiltop Dodoma ambapo jumla ya nyumba 500 zitajengwa katika awamu tofauti. Uamuzi huu umekuja baada ya kukamilika kwa mradi wa awali eneo la Kisasa Relini Njedengwa unaojumuisha nyumba 39 za kawaida pamoja na jengo 1 la biashara  ambapo mauzo yamefanyika kwa mafanikio makubwa. 

Awamu ya kwanza ya Mradi wa Kisasa Hiltop Dodoma inajumuisha nyumba 92 za chini ambapo ujenzi wake ulianza rasmi mwaka 2020 na tayari umekamilika. Hadi sasa 85% ya nyumba zote tayari zimeuzwa. 

Pia kuna ongezeko la nyumba mpya 38 ambapo ujenzi wake unategemewa kukamilika mwezi Septemba 2022 na hivyo kufikisha jumla ya  nyumba 130 katika mradi huu.

Na.

Aina ya nyumba

Idadi ya vyumba

Meta za mraba

Bei

(bila VAT)

Bei (ikiwa na VAT)

1

Aina A

3

115

77,118,644.00

98,500,000.00

2

Aina B

3

85

63,359,322.00

84,500,000.00

3

Aina C

3

78

57,627,118.00

79,800,000.00

4

Aina D

3

68

45,762,712.00

69,800,000.00

5

Aina E

2

60

38,824,630.51

45,800,000.00