Twende na safari na utafute ndoto yako Nyumbani

Watumishi Housing Investments (WHI) ni taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 2014 chini ya sheria ya Makampuni (Cap 212) kwa ajili ya kutekeleza Mpango wa Makazi kwa Watumishi wa Umma na wanachama wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii ambayo ni matarajio katika malengo ya kitaifa na kimataifa kama yalivyoainishwa katika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Makazi (2000), Dira ya Maendeleo ya 2025, na Malengo ya Maendeleo Endelevu:2030. Uwekezaji unafanyika kupita Mfuko wa uwekezaji wa pamoja katika milki(WHI Real Estate Investment Trust Fund au WHI-REIT). Wawekezaji wa awali katika WHI-REIT ni mifuko ya hifadhi ya jamii ikiwemo Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), NHC, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).

MIRADI YA NYUMBA

WATUMISHI NJEDENGWA ESTATE 50%
BUNJU B HOUSING ESTATE 95% 95%
GEZAULOLE RESIDENTS 95%
MKUNDI HOUSING PROJECT 95%
GEZAULOLE RESIDENTS 100%
KISESA HOUSING ESTATE 100%

HUDUMA ZA MSINGI

kupangisha na kuuza nyumba kwa ajili ya makazi na biashara

WHI inauza aina mbalimbali za nyumba ambazo zinakidhi mahitaji ya mteja. Kutokana na chaguo la mteja, nyumba zinapatikana kuanzia zenye vyumba 2 vya kulala hadi vyumba 4, za kujitegemea hadi nyumba zinazotegemeana. Nyumba za WHI zimejengwa kwa kuzingatia Utamaduni wa Mtanzania na maisha ya vijana. WHI ilifanya utafiti wa kutosha katika kubuni michoro ya nyumba ilizojenga hivyo muundo wa nyumba zilizopo imezingatia maoni mbalimbali ya wateja. Kwa maombi maalum, mteja anaweza kuomba kufanyiwa marekebisho katika mchoro wa nyumba anayoitaka.

huduma za uwekezaji

WHI ni Taasisi yenye jukumu la usimamizi wa Mifuko ya uwekezaji ambapo linasimamia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kupitia uwekezaji katika milki (REITs) na Uwekezaji katika Masoko ya Fedha. Uwekezaji katika REITS unafanana na uwekezaji katika Masoko ya hisa. Hadi sasa Mfuko wa Uwekezaji katika Milki (REITS) unamilikiwa na Wawekezaji wa Awali wa WHI na hivyo vipande vyake haviuzwi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hata hivyo katika kipindi hiki cha hali tulivu ambacho kinakadiriwa kuchukua angalau miaka mitatu, vipande vya uwekezaji katika milki vitaweza kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ambapo mwananchi ataweza kupata fursa ya kuwekeza katika Mfuko wa Uwekezaji wa Milki kwa kuuza au kununua vipande kama vile vile inavyofanyika wakati wa kuuza au kununua hisa.

kununua na kupangisha nyumba kwa ajili ya makazi na biashara

WHI inauza aina mbalimbali za nyumba ambazo zinakidhi mahitaji ya mteja. Kutokana na chaguo la mteja, nyumba zinapatikana kuanzia zenye vyumba 2 vya kulala hadi vyumba 4, za kujitegemea hadi nyumba zinazotegemeana. Nyumba za WHI zimejengwa kwa kuzingatia Utamaduni wa Mtanzania na maisha ya vijana. WHI ilifanya utafiti wa kutosha katika kubuni michoro ya nyumba ilizojenga hivyo muundo wa nyumba zilizopo imezingatia maoni mbalimbali ya wateja. Kwa maombi maalum, mteja anaweza kuomba kufanyiwa marekebisho katika mchoro wa nyumba anayoitaka.

huduma za uwekezaji

WHI ni Taasisi yenye jukumu la usimamizi wa Mifuko ya uwekezaji ambapo linasimamia Mifuko ya Uwekezaji wa Pamoja kupitia uwekezaji katika milki (REITs) na Uwekezaji katika Masoko ya Fedha. Uwekezaji katika REITS unafanana na uwekezaji katika Masoko ya hisa. Hadi sasa Mfuko wa Uwekezaji katika Milki (REITS) unamilikiwa na Wawekezaji wa Awali wa WHI na hivyo vipande vyake haviuzwi katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE). Hata hivyo katika kipindi hiki cha hali tulivu ambacho kinakadiriwa kuchukua angalau miaka mitatu, vipande vya uwekezaji katika milki vitaweza kuuzwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ambapo mwananchi ataweza kupata fursa ya kuwekeza katika Mfuko wa Uwekezaji wa Milki kwa kuuza au kununua vipande kama vile vile inavyofanyika wakati wa kuuza au kununua hisa..