MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA

Faida fund ni mfuko wa uwekezaji unaotoa fursa ya kukuza kipato kupitia uwekezaji wa pamoja kwa watanzania hasa wa kipato cha kati na cha chini.

Faida Fund inasimamiwa na Watumishi Housing Investments (WHI) ambayo ni taasisi ya serikali chini ya ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora yenye dhamana ya kusimamia uwekezaji wa pamoja.

Bei ya kipande cha Faida Fund ni shilingi 100/= na unaweza kuanza kuwekeza kuanzisha Shilingi 10,000/= na kuendelea na baada ya hapo unaweza kuwekeza Shilingi 5000/= na kuendelea. Bei ya kipande itapanda kila siku. Utanunua vipande kwa bei ya siku hiyo.

    • Mfuko unaendeshwa na wataalamu waliothibitiwa na Mamlaka ya Mitaji na Masoko (CMSA)
    • Fedha zitakazopatikana zitawekezwa kwenye masoko ya fedha na mitaji yenye kiwango kidogo sana cha hatarishi (Ukwasi)
    • Mfuko upo wazi kwa watanzania na wakazi waliopo ndani na nje ya nchi, watu binafsi, watoto na wawekezaji wa kitaasisi.
    • Unaweza kuwekeza kila mwezi bila makato kutumia standing order au kwa makato ya moja kwa moja kutoka kwa mwajiri, hivyo kukwepa usumbufu.
    • Makato ni madogo sana; hivyo kuwa njia sahihi ya kuwekeza bila gharama kwakuwa unatumia mfumo wa malipo serikalini. (control number)
    • Utaweza kuchukua mkopo na kuweka vipande vyako kama dhamana.
    •  Mfuko unaruhusu uwekezaji kwa watoto.

.

Ndio utaweza kuwekeza kwaajili ya mtoto wako. Mzazi atakua msimamizi wa uwekezaji hadi mtoto atakapofikisha miaka 18.

Kuna njiia kuu 4 za kuwekeza kwenye Faida Fund.

  1. Kwa kupiga *152*00# Kisha chagua Malipo na kuendelea kwa kuchagua WHI na kisha FAIDA FUND
  2. Kwa kutumia mfumo wa fas.whi.go.tz
  3. Kwa kutumia WekezaWHI App
  4. Kwa kujaza fomu zinazopatika ofisi zote za WHI au kwenye tovuti ya www.whi.go.tz

Baada ya usajili, mwekezaji atapatiwa control number ambayo ndio atatumia kununua vipande mara zote. Control number haitabadilika. Utaweza kufanya malipo kwa kutumia simu yako kwa malipo ya serikali, kwa kutumia wakala wa benki au kwa kwenda benki moja kwa moja. Usimpatie mtu hela akununulie vipande.

.

Hakuna gharama zozote katika kujiunga au kujitoa. Matumizi ya mtandao wa serikali (GePG) yanafanya mfuko huu kuwa ndiyo mfuko nafuu zaidi kuwekeza na hivyo kumuwezesha muwekezaji kupata faida zaidi kwa uwekezaji wake. 

Vipande vya faida fund ni mali yaani kama hakimiliki zingine. Ni asset pia. Hivyo basi endapo mmiliki atafariki basi warithi wake wataridhi hivo vipande kupitia msimamizi wa mirathi au kama kulikua na wosia ambao umeelekeza vipande virithiwe na nani basi hilo litasimamiwa na msimamizi wa mirathi. Faida Fund baada ya kupokea nyaraka za mahakama za uteuzi wa msimamizi wa mirathi  itakamilisha mchakato wa urithi wa vipande hivyo.

Fedha zote za Faida Fund zinasimamiwa na Benki ya CRDB.

Ndio, Mwekezaji anaweza akamwambia mwajiri amkate mshahara wake na kuweka moja kwa moja kwenye mfuko wa Faida Fund (Standing order).

Vipande vinauzwa au kununuliwa kutokana na bei ya vipande iliyotangazwa kwa siku husika (NAV). Wawekezaji wanashauriwa kufuatilia bei ya kipande iliyotangazwa kwa siku husika waliyonunua vipande.

Unaweza kuuza vipande vyako baada ya miezi 3 toka kujiunga kwenye mfuko wa Faida Fund.

Utapata fedha zako ndani ya siku 3 za kazi toka kuomba malipo.