FAIDA FUND

Mfuko wa Faida ni mpango ulio wazi unaotoa fursa nyingine ya uwekezaji kwa Watazania hasa wa kipato cha kati na cha chini kupitia uwekezaji katika vipande ili kupata mapato shindani kupitia ukuaji wa mitaji; na kutengeneza utamaduni wa kuwekeza katika Masoko ya Fedha na Mitaji. Mfuko wa Faida ulifunguliwa mwezi Novemba 2022. Mfuko unatarajiwa kujumuisha wawekezaji wadogo wakiwemo bodaboda, wanafunzi, wafanyakazi, wastaafu, wakulima n.k. Mfuko wa Faida umesajiliwa na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) mwezi Septemba 2020.

Mfuko huu unaendeshwa na WHI kama Msimamizi wa Mfuko kwa kutumia wataalam waliosajiliwa na CMSA. Mfuko huu unaimarisha ukuaji wa mtaji na kuongeza faida kupitia sera ya uwekezaji.

Uwekezaji unafanyika katika dhamana za muda mfupi kama vile Ankara za Hazina, hati za amana za serikali na uwekezaji wa Benki wa muda mfupi n,k

Mfuko huu uko wazi kwa Watanzania na Wakazi waliopo ndani na nje ya nchi, unahusisha watu binafsi (ikijumuisha watoto), na wawekezaji wasio watu binafsi kama Mifuko ya Pensheni, Mabenki/Mashirika Taasisi za Serikali, Mamlaka za Udhibiti, Vyombo vya ulinzi na usalama, Asasi zisizo za kiserikali na Mashirika mengineyo n.k.

Kiwango cha chini cha awali cha uwekezaji niĀ  kuanzia TSh 10,000/= na kuendelea na mauzo yanayofuata baada ya mauzo ya awali ni kuanzia Tsh 5,000/= na kuendelea.

Hakuna kiwango cha juu cha kuwekeza.

Fedha hizo zitawekezwa kwenye Masoko ya Fedha na Mitaji yenye kiwango cha chini cha hatari za uwekezaji.

Mwekezaji hatatozwa gharama yoyote ya kujiunga au kujitoa katika mfuko.

Uuzaji wa vipande utafanyika kila siku baada ya miezi mitatu tangu kumalizika kipindi cha mauzo ya awali. Mfuko utatuma malipo ya mauzo ya vipande ndani ya siku tatu za kazi baada ya kupokea maombi katika Makao Makuu ya Watumishi Housing Investments. Fedha za mauzo zitatumwa moja kwa moja katika akaunti ya benki ya mwekezaji au simu ya mkononi iliyosajiliwa.

Kwa mujibu wa sheria za nchi, mgawanyo wa mapato ya Mfuko yamesamehewa kodi ya mapato kwa wawekezaji.

Vipande vinauzwa au kununuliwa kutokana na bei ya vipande iliyotangazwa kwa siku husika (NAV). Wawekezaji wanashauriwa kufuatilia bei ya kipande iliyotangazwa kwa siku husika waliyonunua vipande.

Kila mwekezaji anayekidhi vigezo vya kujiunga na Mfuko anaweza kusajiliwa kupitia njia zifuatazo:

1. Kujiunga moja kwa moja kupitia mtandao kwa njia zifuatazo:

    (a) Tovuti ya WHI kwa kubonyeza hapa

    (b) Kutumia simu ya mkononi (USSD) kama ifuatavyo:

           Piga *152*00#
           Chagua 1. Malipo
           Chagua 6. WHI
           Chagua 1. Tengeneza Akaunti ya Binafsi
           Kisha fuata maelekezo jinsi ya kujisajili.

    (c) Kutumia App ya WekezaWHI kupitia simu janja.

2. kupitia kujaza fomu ya kujiunga inayopatikana:

    (a) Makao Makuu ya Ofisi za WHI au katika ofisi za matawi

    (b)  kwa kupakua fomu moja kwa moja kutoka kwenye tovuti ya WHI kwa kubonyeza hapa

Ratiba ya mauzo ya awali ya vipande vya MFUKO WA FAIDA kwa umma ni kama ifuatavyo: –

a)   Uzinduzi wa mauzo ya awali: 01 Novemba, 2022
b)   Mwisho wa mauzo ya awali: 31 Disemba, 2022
c)   Mauzo kutokana na matangazo ya bei za vipande 02 Januari, 2023
  1. Uidhinishwaji wa daftari la Wawekezaji kupitia Mamlaka ya Uwekezaji wa Mitaji na Dhamana (CMSA):     05 Januari, 2023
  2. Tangazo la Matokeo ya uwekezaji:                            10 Januari, 2023
  3. Uzinduzi rasmi wa Mfuko:                                           14 Januari, 2023
  4. Tarehe ya kuanza kuuza vipande:                               01 April, 2023